RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA ROBERT MUGABE


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye ameaga dunia nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu.

Magufuli kupitia akaunti yake ya Twitter amemwelezea Mugabe kuwa alikuwa kiongozi shupavu, jasiri ambaye aliupinga na kuukataa ukoloni kwa vitendo.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. 

"Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa  Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina."


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527