Picha : NYOKA MKUBWA AVAMIA MKUTANO WA WAZIRI MKUU IRINGA.....ASKARI POLISI ALIYEMDHIBITI APEWA ZAWADI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 28, 2019

Picha : NYOKA MKUBWA AVAMIA MKUTANO WA WAZIRI MKUU IRINGA.....ASKARI POLISI ALIYEMDHIBITI APEWA ZAWADI

  Malunde       Saturday, September 28, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Septemba 28, 2019. 

Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post