OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATOA ELIMU YA UDHIBITI WA KEMIKALI ZINAZOHARIBU TABAKA LA OZONI KWA MAOFISA FORODHA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 18, 2019

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATOA ELIMU YA UDHIBITI WA KEMIKALI ZINAZOHARIBU TABAKA LA OZONI KWA MAOFISA FORODHA

  Malunde       Wednesday, September 18, 2019

Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Faraja Ngerageza amesema kuwa  Matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi zaidi ya urujuani (UV-B) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali.  Ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua  warsha ya mafunzo kwa Maafisa forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kuhusu udhibiti wa kemikali zinazoharibu tabaka la ozoni.

Aliongeza kuwa, Wanasayansi duniani wamethibitisha kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, upungufu wa  uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi hivyo mtu aweza kuonekana mzee kuliko umri wake. Pia watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya. Madhara mengine ni pamoja na kuharibu fiziolojia ya mimea na michakato ya ukuaji wake na kusababisha mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kusababisha mabadiliko ya bioanuwai katika ikolojia mbalimbali


Aidha katika kuhakikisha kuwa jukumu hili chini ya Sheria ya Mazingira linatekelezwa na kusimamiwa ipasavyo Ofisi ya Makamu wa Rais  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa forodha imekuwa ikijitahidi kujenga uwezo wa Taasisi mbalimbali katika kusimamia Kanuni za Udhibiti wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni za mwaka 2007 pamoja na kutoa vifaa katika mipaka yetu vinayowezesha kutambua gesi  hizi zinapoingizwa nchini. 

Ofisi ya Makamu wa Rais imekua na utaratibu wamara kwa mara  kuandaa warsha ya mafuzo kwa Maafisa Forodha na Wasimamizi wa sheria Nchini kote kuhusu udhibiti wa kemikali  ambazo zinzingizwa Nchini zinazoharibu tabaka la ozoni.   Warsha hiyo imehudhuriwa na Maafisa forodha wa mipaka yote Nchini kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post