KUTANA NA NYOKA WA AJABU..ANA VICHWA VIWILI,MACHO MANNE....ANAVIMBA BALAA

Nyoka mwenye vichwa viwili aliyepewa  jina 'Double Dave' amepatikana katika msitu mmoja uliopo jimbo la New Jersey, nchini Marekani. 

Kwa mujibu wa ABC News, Marekani, nyoka huyo ana umbo dogo na mwenye sumu kali. 

Licha ya kuwa na vichwa viwili vilivyokamilika, Double Dave ana macho manne na ndimi mbili ambazo zinafanya kazi tofauti. 

Pia ana uwezo wa kujibadilisha na kuvimba anapokumbana na adui.

Ripoti inaendelea kusem kuwa, Schneider ambaye ni mtaalam wa wanyama wanaotambaa, alisema yeye na mtaalam mwenzake walimwona nyoka huyo Agosti 25, 2019 na wakampa jina la Double Dave kwa sababu yeye Schneider na mwenzake wote majina yao ni David. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527