RC GAGUTI AIOMBA BENKI YA NMB KUWAPUNGUZIA RIBA WALIMU KAGERA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 24, 2019

RC GAGUTI AIOMBA BENKI YA NMB KUWAPUNGUZIA RIBA WALIMU KAGERA

  Malunde       Tuesday, September 24, 2019
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti ameiomba benki ya NMB mkoani Kagera kuwapunguzia riba walimu kufuatia kuwa wadau wakubwa wa benki hiyo kwa muda mrefu.


Mkuu wa mkoa Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ametoa kauli hiyo leo Septemba 24,2019 wakati akifungua kongamano la Walimu na Benki ya NMB lililofanyika katika ukumbi wa Elct Hotel uliopo manispaa ya Bukoba Mkoani hapa.

Mhe. Gaguti amesema Benki hiyo inapaswa kuangalia na kuona umuhimu mkubwa kwa walimu hao kwa kuwapunguzia riba kufuatia kuwa wadau wakubwa wa kwa taasisi hiyo kwa kipindi kirefu .

Amesema kutokana na walimu hao kuipa kipaumbele benki hiyo katika huduma hiyo kwa muda mrefu benki hiyo haina budi kuweka unafuu kwa walimu hao.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka walimu hao kuhakikisha wanatanua wigo kwa kuunda vikundi vya pamoja katika Kata zao na kuomba mikopo ya miradi mikubwa na ya pamoja ili kuinua vipato vyao hasa pale wanapostaafu. 

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewahimiza walimu hao kuwa mabarozi wazuri katika kuchangia kodi na kuhimiza wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa ya aina yotote jambo litakalosaidia kuongeza pato la nchi.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Gabulanga iliyopo wilayani Missenyi mkoani hapa Mutalemwa Makwabe kwa niaba ya Walimu wenzake amesema kuwa wanaishukuru benki hiyo kwa namna inavyoendelea kuwajali walimu pamoja na kutoa misaada mbalimbali katika shule huku akidai kuwa shule yake iliwahi kupatiwa misaada mbali mbali na benki hiyo ikiweno madawati na mbao.

Naye Meneja wa Benki ya NMB kanda ya ziwa Ibrahimu Agustino amesema kuwa benki hiyo inatenga 1% kila mwaka katika kuihudumia jamii na kuongeza kuwa ndani ya mwaka huu tayari zimetengwa shilingi bilioni moja ambapo hadi sasa wametoa zaidi ya milioni mia sita katika kusaidia jamii.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti akizungumza na walimu pamoja na wanafanyakazi wa NMB Kagera katika kongamano hilo

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post