WALIMU 16 MATATANI KWA KURUHUSU MWANAFUNZI FEKI AFANYE MTIHANI WA DARASA LA SABA 2019 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 12, 2019

WALIMU 16 MATATANI KWA KURUHUSU MWANAFUNZI FEKI AFANYE MTIHANI WA DARASA LA SABA 2019

  Malunde       Thursday, September 12, 2019
Walimu 16 wa Shule ya Msingi Kenyamanyori halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara wamekamatwa na polisi kwa madai ya kumruhusu anayedaiwa kutokuwa mwanafunzi kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba.

Walimu hao waliopangiwa kusimamia mitihani katika shule mbalimbali, walijikuta wakitakiwa kukabidhi bahasha za mitihani na fedha walizopewa kwa ajili ya kusimamia kisha kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 12, 2019 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa amesema, “Ni kweli tukio hilo lipo, wamekamatwa inaonekana kuna namna na walishirikiana.”

Chanzo cha taarifa hizo kinaeleza kuwa walimu hao walibainika baada ya taarifa kutumwa ofisi za elimu Mkoa wa Mara kuwa kuna mwanafunzi feki miongoni mwa wanaofanya mtihani huo ulioanza jana na kumalizika leo.

Via Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post