MLIPUKO WAUA NA KUJERUHI WAWILI PWANI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 21, 2019

MLIPUKO WAUA NA KUJERUHI WAWILI PWANI

  Malunde       Saturday, September 21, 2019

Hali ya taharuki imejitokeza katika eneo la Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani kufuatia mlipuko mkubwa wa kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu na kusababisha kifo cha mtu mmoja mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Mbaraka Koromera mwenye umri wa miaka 37.

Aidha katika mlipuko huo uliotokea Msangani, watu wengine wawili Fatuma Likupila maarufu mama Tabu, na Shomari Athumani walikimbizwa katika hospitali ya Tumbi baada ya kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mlipuko huo, Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa marehemu alifariki kwa mlipuko huo uliotokea, mishale ya saa tano Asubuhi Septemba 20, 2019.

Chuma hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilimlipukia wakati akichambua vyuma chakavu kwenye nyumba isiyoisha (pagale) inayomilikiwa na Rajabu Ally Nyangale.

Aidha Kamanda Wankyo ameongeza kuwa katika tukio hilo Fatuma Likupila maarufu mama Tabu, amepata majeraha katika maeneo ya kichwani na kwamba hali yake ni mbaya alikuwa akitokwa damu masikioni huku mwengine Shomari Athumani akijeruhiwa mwili mzima baada ya kuchomwa na vitu vyenye ncha kali yaliyomsabababishia jeraha kubwa mapajani na sehemu za tumboni.

Kufutia kutokea kwa tukio hilo timu ya waatalamu kutoka Jeshi la Polisi na kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaendelea na uchunguzi, ili kubaini mlipuko huo kama ni bomu na ni aina gani ya bomu huku jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani likitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pale wanapoona vitu vyenye mashaka ili kuepuka madhara kama yanayoweza kujitokeza.
Chanzo - EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post