MKUU WA WILAYA YA HAI, LENGAI OLE SABAYA AAMURU VIONGOZI WANNE WA CHADEMA WAKAMATWE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 20, 2019

MKUU WA WILAYA YA HAI, LENGAI OLE SABAYA AAMURU VIONGOZI WANNE WA CHADEMA WAKAMATWE

  Malunde       Friday, September 20, 2019

Mkuu wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya ameagiza viongozi wanne wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy Owenya kukamatwa baada ya kutembelea shule ya Sekondari Rundugai wilayani humo kwa madai ya kufanya siasa kinyume cha utaratibu.Wengine waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, Katibu wa Mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini, Clement Kwayu.

Sabaya amesema kuwa viongozi hao walikwenda katika shule hiyo leo Ijumaa asubuhi kwa madai ya kuzungumza na wanafunzi na kutoa misaada, bila mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na taarifa.Amesema, kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali,yeyote anayetaka kutoa misaada katika shule yeyote atoe taarifa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ili misaada hiyo ijulikane lengo lake na iweze kuratibiwa


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post