BENKI YA MKOMBOZI YAMSAIDIA MGONJWA WA SARATANI


Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Nwaka Mwabulambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomtembelea Bw,Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi na kutoa mchango wa sh. miloni moja kwaajili ya matibabu pia nakumfungulia akaunti ya pamoja (Joint Akauti) kulia ni Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid,Meneja Mikopo wa Benki hiyo Bw. Andrew Chimazi.
Bi-Fatuma Rashid (katikati) akiushukuru uongozi wa benki 
hiyo kwa mchango wao walioutoa (kulia) Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge, na Mkurugenzi wa Hazina wa benki hiyo , Nwaka Mwabulambo.
Meneja wa Benki ya Biashara ya Mkombozi, Tawi la Kariakoo, Bonphace Mahenge (kushoto), akimshuhudia, Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid (katikati) akijaza fomu kwa alama ya kidole kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akaunt) kwa ajili ya michango ya kumsaidia.Uongozi wa benki hiyo ulimtembelea, Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi baada ya kuona matangazo kwenye vyombo vya habari. 
Bi-Fatuma Rashid akiwa na mume wake Bw.Salim Rashid ayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi.
Uongozi wa benki hiyo ukishauriana jambo ulipomtembelea Bw.
 Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam anayesumbuliwa na ungonjwa wa saratani ya ulimi. 

(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON) 

BENKI ya Biashara ya Mkombozi imeahidi kuendelea kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa kuchangia watu wenye mahitaji maalumu.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa benki hiyo kutoa msaada kwa familia ya Salim Rashid mkazi wa Tuangoma Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mara baada ya kutembelea familia hiyo Nwaka Mwabulambo Mkurugenzi wa Hazina wa Benki hiyo alisema kuwa katika kuelekea miaka kumi ya benki hiyo bebki imeamua kushiriki na familia hiyo kwa kutoa msaada wa kuwafungulia akaunti ili jamii iweze kuwasaidia.

Alisema baada ya kupata taarifa kutoka katika vyombo mbalimbali kuhusu uhitaji wa Rashid ambaye anasumbuliwa na saratani uongozi wa benki uliamua kushiriki kwa vitendo kwa kuisadia familia hiyo kwa kutoa mchango wa sh. miloni moja sambamba na kufungua akaunti ya pamoja ili kuirahisishia familia hiyo kwenye zoezi la ukusanyaji wa fedha za msaada kutoka kwa jamii.

“Kama tunavyofahamu simu za mkononi zina ukomo wa utoaji fedha hivyo benki kwa kuliona hilo tumeamua kuirahisishia jamii kazi hii kwa kufungua akaunti ya pamoja (Joint Akauti) ambayo itawezesha jamii na taasisi mbalimbali kuchangia kiasi chochote cha fedha ili kuirahisishia  familia hii iweze kupata msaada
wa fedha za matibabu,”alisema Mwabulambo

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kushiriki shughuli za kijamii benki itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuchangia shughukli mbalimbali za kijamii kama njia ya kutoa shukrani kwa kile wanachokipata kutoka kwa wateja wao ambao ndiyo wadau.

Aidha aliongeza kuwa tayari uongozi wa benki umewashawishi watumishi wake kuona umuhimu wa kuchangia matibabu ya Rashidi huku ikiwataka watanzania wengine kuona umuhimu wa kutoa michango kwa familia hii na zinmgine zenye mahitaji .

Aliitaja akaunti namba ambayo watanzania wanaweza kutoa michango yao kwa familia hiyo kuwa ni 00420111912801 na kusema kuwa kufanya hivyo kutarahisisha matibabu ya Rashid ambaye tayari alishaanza matibabu hapa nchini na nje ya nchi.

Kwa upande wake Fatuma Rashid mke wa Salim Rashid aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa mchango wao na kuwaomba kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha matibabu zaidi ya Rashid.

“Nashukuru Benki ya Ukombozi kwa kuliona tatizo la mume wangu na kulichukulia uzito kwa kuchangia kiasdi hicho
cha fedha sambamba na kufungua akaunti, hii imetupa moyo kuwa jamii ipo pamoja nasi,”alisema Fatuma.

“Kama Benki tumeitembelea familia hii ya Rashid ili kuifariji na tumeshaifungulia akaunti ya pamoja itakayowezesha jamii kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwezesha matibabu ya Salim ambaye anasumbuliwa na saratani,”alisema na kuongeza kuwa hii pia itasaidia taasisi mbalimbali kuweza
kuchangia zaidi matibabu hayo.

Hata hivyo aliwaomba watanzania wote wenye mapenzi mema kuwa karibu na familia hiyo ili kuwezesha matibabu
yaanyike na kuimarisha afya ya mume wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527