HALMASHAURI YA BUKOBA,ASASI, WANANCHI WAPANDA MITI MILIONI 1.8

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukoba Solomoni  Kimilike

Na Ashura Jumapili, Bukoba.
Katika kutunza na kuhifadhi mazingira halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera kwa kipindi cha mwaka 2018/2019  kwa kishirikiana na wananchi pamoja na asasi mbalimbali imepanda jumla ya miti 1,836,342.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Solomoni  Kimilike Agost  4 mwaka huu katika kikao cha baraza la  madiwani wa halmashauri hiyo.

Kimilike, alisema lengo lilikuwa kupanda miti  1,500,000 ambapo  miti  1,743,189 inaendelea kustawi.

Alisema wananchi wamehamasishwa kupanda miti  rafiki na kutunza mazingira katika maeneo yao.

Alisema halmashauri kwa kushirikiana na tume  ya Taifa ya mpango wa matumizi bora ya Ardhi wananchi wa Vijiji 8 wanaweza kupimiwa na kumilikishwa maeneo yao kwa njia ya hati miliki za kimila.

Alisema kwa kipindi cha robo  hii wamepima na kumilikisha mashamba 8.

Alisema mpango wa urasimishaji  shirikishi jamii wamepima viwanja 25 katika eneo la  Katoro na uhamasishaji wa wananchi kuandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi unaendelea katika vijiji vyote.

Alisema hadi sasa Vijiji 73 vimehamasishwa kati ya Vijiji 94 vya halmashauri hiyo na zoezi linaendea kwa Vijiji vingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527