MADEREVA BAJAJI WAFUNGA BARABARA MOROGORO....JESHI LA POLISI LAWATULIZA


Baadhi ya madereva wa bajaji mjini Morogoro wamelazimika kufunga barabara kufuatia kamatakamata ya polisi iliyofanyika katika mji huo mapema leo.

Madereva hao wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya askari polisi na askari wa akiba kuzingira katika maeneo mbalimbali ya katikati ya mji pamoja na kituo cha daladala na kuzikamata bajaji zao.

Hatua hiyo ikakilazimu kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro kikiongozwa na Kamanda Michael Daleli kuingilia kati na kufanikiwa kutuliza ghasia pamoja na kuondoa msongamano uliosababisha shughuli mbalimbali kusimama.

"Barabara iligeuzwa kuwa kituo cha maegesho ya bodaboda na bajaji, sasa tunazifungua na nyinyi ni mashahidi hata misafara iliyokuwa inapita eneo hili ilikuwa inazunguka mbali sana kuelekea pale Ikulu ndogo", amesema Kamanda Daleli.

Naye Mratibu wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA, Mhandisi Godwin Mpinzile amesema kuwa madereva hao walipewa sehemu za kwenda kuegesha magari yao lakini wamekuwa wakikaidi na ndiyo maana zoezi hilo limefanyika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527