WAANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI NA KUFUATA SHERIA ZA NCHI WAKATI WA UCHAGUZI


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani Kagera Mbeki Mbeki akizungumza na waandishi wa habari wilayani Misenyi
Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani Kagera Mbeki Mbeki akisalimiana na Katibu Tawala wilaya ya Misenyi Abdallah Mayomba.

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog 
Waandishi wa habari mkoani Kagera wamekumbushwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kufuata sheria za nchi katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki.

Rai hiyo imetolewa Septemba 16, 2019 na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani Kagera Mbeki Mbeki wakayi akizungumza na waandishi wa habari wilaya ya Misenyi ambapo amesema ni lazima waandishi wa Habari watambue kuwa wafanya kazi chini ya sheria za nchi.

Amesema ni vyema waandishi wa habari wakaepuka kuandika habari zinazoegemea upande mmoja au habari za uchochezi ambazo haziwezi kuleta matokeo chanya katika jamii.

Naye Katibu Tawala wilaya ya Misenyi Abdallah Mayomba amesema serikali wilayani humo itahakikisha inakuwa bega kwa bega na waandishi wa habari ikiwemo kutoa ufafanuzi wa mambo yatakayohitaji kuhabarisha wananchi. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527