MWALIMU WA SHULE YA LITTLE TREASURES AFARIKI KWA KUJIRUSHA GHOROFANI ' NIGHT CLUB LEVEL FOUR' SHINYANGA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog

Mwalimu wa Shule ya Msingi Little Treasure iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga,Erick Adams (37) mkazi wa Bugayambelele amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne ya Night Club ya Level Four Mjini Shinyanga.


Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Septemba 22,2019 majira ya saa 12 na dakika 10 katika Jengo Jipya la NSSF ilipo Night Club ya Level Four Shinyanga Mjini.

"Mwalimu Erick Adams wa Shule ya Msingi Little Treasure na mkazi wa Bugayambelele alijirusha kutoka ghorofa ya nne ya Night Club ya Level Four na kufariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu",amesema Kamanda Abwao. 

"Chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.Mbinu iliyotumika ni kujirusha kutoka ghorofa ya Nne alipokuwa akinywa pombe hadi chini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ukisubiri kukabidhiwa kwa ndugu",ameongeza.

Kamanda Abwao ametoa  wito kwa wamiliki wa kumbi za starehe zilizopo katika majengo ya ghorofa, kuchukua tahadhari za kiusalama kwa wateja wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527