WATAALAMU WASHINDA TUZO KWA UCHUNGUZI WAO KUHUSU JOTO LA KORODANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 13, 2019

WATAALAMU WASHINDA TUZO KWA UCHUNGUZI WAO KUHUSU JOTO LA KORODANI

  Malunde       Friday, September 13, 2019

Watafiti walifanya ukaguzi kwa kugusa korodani za kushoto na kulia za wahudumu wa posta na madereva wa basi ishirini na wawili.Utafiti uliofanywa kupima iwapo kuna tofauti ya ujoto kati ya korodani la kushoto na la kulia ni mojawapo ya ulioshinda tuzo bandia za Nobel mwaka huu.

Wataalamu wa masuala ya uzazi Roger Mieusset na Bourras Bengoudifa walipima joto katika korodani za wahudumu wa posta, wakiwa uchi wa mnyama na wakiwa wamevaa nguo.

Waligundua ya kwamba la kushoto lina joto zaidi, iwapo mwanamume amevaa nguo.

Tuzo hiyo ya mzaha ilitangazwa katika hafla kwenye chuo kikuu cha Harvard.

Katika utafiti wao "Ujoto wa umbo la korodani la binaadamu" uliochapishwa katika jarida la Human Reproduction, watafiti hao walifafanua kuwa utafiti wao ulihusisha kupima joto la korodani kwa mguso kila baada ya dakika mbili.

Waliwaomba wafanyakazi 11 wa posta wasimame kwa saa moja na nusu wakati wakiwapima joto katika korodani zao.

Katika utafiti mwingine, walipima joto lililopo kwa madereva 11 wa basi wakati wakiwa wamekaa chini.

Tuzo hiyo ya mzaha ya Nobel ni zawadi inayochapishwa katika 'Annals of Improbable Research' lakini baadhi ya mada zinazotambuliwa katika tuzo hiyo, huwa zina umuhimu ndani yake.

Katika utafiti huu, utafiti mwingine umeashiria kuwa joto katika sehemu ya korodani linaweza kuathiri uwezo wa mwanamume kuzalisha.

Kiwango cha manii kwa wanaume katika mataifa ya magharibi kinapungua, lakini ni machache yanayofahamika kuhusu namna ya kuliimarisha hilo.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post