Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari nchini Tanzania (UTPC) umeitangaza Kampuni ya Jamii Forums kuwa mshindi wa Tuzo ya Mwangosi mwaka 2019.Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019,Charles Kayoka ameitangaza Jamii Forums kuwa mshindi wa Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019 katika mkutano uliohudhuriwa viongozi wa Klabu za Waandishi wa habari nchini pamoja na wageni mbalimbali katika ukumbi wa Raha Leo,Zanzibar leo Septemba 6,2019 ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi,Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums na mwanzilishi wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo leo katika ukumbi wa Raha Leo,Zanzibar . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums, Maxence Melo akiangalia tuzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums, Maxence Melo akionesha tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Jamii Forums, Maxence Melo akionesha tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 10 Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media inayomiliki Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Mello kwa kushinda tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Mkurugenzi Mkuu Jamii Forums, Maxence Melo akipokea hundi ya shilingi milioni 10 ambayo ni zawadi ya Tuzo ya Daudi Mwangosi 2019.
Social Plugin