IRAN YAIKOSOA MAREKANI KWA KUMYIMA RUHUSA WAZIRI WAKE WA MAMBO YA NJE JAVAD ZARIF KUMTEMBELEA HOSPITALINI BALOZI WA IRAN


Iran imeikosoa Marekani kwa uamuzi wa kikatili wa kumzuia waziri wake wa mambo ya kigeni Javad Zarif kumtembelea hospitalini Balozi wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa Majid Takht Ravanchi anaetibiwa ugonjwa wa saratani mjini New York. 

Zarif anahudhuria mkutano wa kilele wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini humo. 

Shirika la habari la kitaifa nchini humo IRNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya kigeni Abbas Araghchi akisema Marekani imeligeuza suala hilo la kibinaadamu kuwa la kisiasa. 

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema itamruhusu iwapo Iran itamuachia huru mmoja wa raia wengi wa Marekani wanaodaiwa kushikiliwa kimakosa nchini Iran. 

Mwezi Julai Marekani ilitangaza kumzuia waziri huyo kuingia nchini humo, ikiwa ni miongoni mwa vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo.

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527