MSANII H BABA, AHAMISHIA NGUVU ZAKE KWENYE SOKA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, September 23, 2019

MSANII H BABA, AHAMISHIA NGUVU ZAKE KWENYE SOKA

  Malunde       Monday, September 23, 2019

Na Fabian Fanuel, Mwanza.
MSANII Maarufu wa Muziki wa Bongo Flava asiyechuja kutoka Mabatini Mwanza H Baba ameendeleza utaratibu wake wa kusapoti timu za Mwanza kwa kuanzisha utaratibu wa kuchangisha pesa kutoka kwa mashabiki Pindi timu hizo zinapocheza na timu zingine katika Viwanja vya Nyamagana na CCM Kirumba Mwanza.


Akizungumza Mara baada ya kuasisi michango hiyo, H Baba alisema ameanzisha zoezi hilo akiwa na jukumu moja la kuhamasisha mashabiki wote wanaongia uwanjani kusapoti timu za Mwanza.

Mmoja Kati ya Wanachama wa Pamba FC ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula alisema mkakati huo wa kuchangisha fedha kwa ajili ya timu za Mwanza ni suala zuri na linapaswa kuungwa mkono na kila mwana Mwanza.

Akimkabidhi Nahodha Msaidizi wa Pamba FC Nizar Khalfan, Mabula alisema wataendelea na zoezi hilo lililoasisiwa na H Baba kwa timu zote za Mwanza, kusudi likiwa ni kuongeza hamasa kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Pamba FC inakuwa timu ya tatu kuchangiwa baada ya Alliance FC, Mbao Fc na leo Pamba FC, ambapo jumla ya 173,000 imepatikana katika mchango huo na kumkabidhi wachezaji wa timu hiyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post