DEREVA TAKSI KESI YA MO DEWJI AENDELEA KUSOTA....WATUHUMIWA WENGINE BADO WANASAKWA


Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili dereva taksi mkazi wa Tegeta, Mousa Twaleb (46) ya uhujumu uchumi ikiwamo kusaidia kutendeka uhalifu, kutakatisha Sh. milioni nane na kumteka Mohamed Dewji maarufu kama ‘Mo’ umedai kuwa bado unaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanne kwa ajili yakuwaunganisha katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, na kwamba bado upande wa Jamhuri unaendelea na juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wengine.

Alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Hakimu alisema kesi hiyo itatajwa tena Septemba 30, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527