Picha : MAHAFALI YA 13 YA SHULE ZA ALLIANCE YAFANA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 24, 2019

Picha : MAHAFALI YA 13 YA SHULE ZA ALLIANCE YAFANA

  Malunde       Tuesday, September 24, 2019
Na Fabian Fanuel - Malunde 1 blog Mwanza.

Wanafunzi waliohitimu mtihani wao wa Darasa la Saba kutoka Shule za Alliance zilizoko Mwanza wameaswa kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao ili Kufanya vizuri katika Elimu yao.


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Mwanza ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye mahafali ya 13  ya wanafunzi wa Shule za Alliance, Yona Alfred katika sherehe hizo zilizofanyika Katika viwanja vya Shule za Alliance.

Bwana Alfred aliwaaasa wanafunzi wote waliomaliza mtihani yao ya Darasa la Saba shuleni hapo kuwa, hakuna kitu kizurii ambacho watafanya maishani Kama kuongeza nguvu na juhudi kwenye masomo yao.

Alisema anaamini wanafunzi hao watafanya vizuri kwenye mitihani yao waliyofanya Kutokana na historia ambayo imekuwa nayo Shule za Alliance, maana wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani yote ya kitaifa na mengine.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shule za Alliance James Marwa Bwire ambaye pia ni Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, alisema kuwa Uongozi wa Shule hizo umewapa nafasi waalimu kuwafundishi wanafunzi hao vizuri, umetimiza Mahitaji ya waalimu na kuwaandaa wanafunzi kwa mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma na wanaamini kuwa watafanya vizuri kwenye mitahani yao.

Mmoja Kati ya Waalimu Mkuu wa Shule za Alliance John Marwa alisema wametekeleza kazi yao vizuri na wanaamini wanafunzi wao watapata matokeo mazuri kulingana na umakini wao wa kufundisha na kuwaandaa wanafunzi hao kwa mitihani hiyo ya kitaifa.

Katika kuonyesha Shule Alliance zinawapa wanafunzi nafasi ya michezo Mwenyekiti Msaidizi wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Alliance FC Nyaitati Stephano aliwashukuru wadhamini wote waliowekeza katika hiyo ili ipate kupata matokeo chanya.

Wadhamini ambao wanadhamini Timu ya Alliance FC ni Shule za Alliance Schools, Access Bank, Emirate Alluminium Profile na Mwanza Pure Drinking Water.

Mahafali ya Kumi na Tatu ya Shule za Alliance yalifanyika Juzi katika viwanja vya Shule za Alliance wakishirikisha wahitimu Kutoka Shule za Alliance Primary School wanafunzi 24, New Alliance Primary School wanafunzi 24 na Bwire International School wanafunzi 41.
Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Nyamagana Yona Alfred akizungumza kwenye  mahafali ya 13  ya wanafunzi wa Shule za Alliance, Yona Alfred katika sherehe hizo zilizofanyika Katika viwanja vya Shule za Alliance. 
Picha zote na Fabian Fanuel - Malunde 1 blog Mwanza.
Mwanafunzi smart Denis Tarimo akipokea cheti chake.
Msafara wa wahitimu ukiongozwa na vijana wa scout kuingia kwenye viwanja vya mahafali.
Msafara wa wahitimu ukiongozwa na vijana wa scout kuingia kwenye viwanja vya mahafali.
Wahitimu wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Wahitimu wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Wahitimu wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Wahitimu wakifuatilia hotuba mbalimbali.
Wanafunzi wa pre school(chekechea) wakitumbuiza
Wanafunzi wa pre school(chekechea) wakitumbuiza
Wanafunzi wa pre school(chekechea) wakitumbuiza
Mkurugenzi wa Shule za Alliance James Marwa Bwire akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Shule za Alliance James Marwa Bwire akizungumza kwenye mahafali hayo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post