Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ya vijana Duniani ambapo huadhimishwa Agosti 12 kila mwaka ambapo kwa Tanzania Maadhimisho hayo kwa Mwaka 2019 yamesogezwa mbele hadi Agosti 15 na 16,2019 ,Zaidi ya vijana 500 kutoka Tanzania wanatarajia kukutana jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari leo Agosti ,14,2019 Jijini Dodoma ,Meneja Mradi wa shirika la Kimataifa la idadi ya Watu [ UNFPA] kwa Tanzania , katika kitengo cha Maendeleo ya vijana Dkt. Majaliwa Marwa amesema mwaka huu itakuwa ni kutimiza miaka 20 tangu maadhimisho hayo kuanzishwa maadhimisho hayo
Ametaja Malengo ya Maadhimisho hayo kuwa ni pamoja na kupanua wigo uelewa juu ya vijana pamoja na changamoto zinazowakabili na Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa na mada zitakazowasilishwa ni pamoja na na elimu ya uzazi kwa vijana pamoja na changamoto za ajira kwa vijana.
Kwa Upande wake,Mwakilishi wa Shirika linaloratibu masuala ya vijana Tanzania[Restless Development] Bw.Ridhione Juma amesema shirika hilo litahakikisha kuwa na ulinganifu kwa makundi ya watu maalum ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu huku katibu wa Asasi ya Vijana Tanzania [AFriYAN] akiishukuru Serikali ya Tanzania kwa Kutoa Elimu Bure.
Afisa Mawasiliano wa shirika la Kazi Duniani [ILO]kwa Afrika Mashariki Bw.Magnes Minja amesema utafiti uliofanyika mwaka 2014 ulibaini kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana ilikuwa asilimia 11.7& ikilinganishwa na ukosefu wa asilimia 10.3 % kwa ukosefu wa ajira kiujumla huku meneja mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa[UN]Bi.Stella Vuzo akisema ajenda kuu ya Umoja wa Mataifa ni Malengo ya Maendeleo endelevu.
Naye Mwakilishi wa UN Kitengo cha Habari nchini Tanzania ,Dokta.Warren Bright Hasheem amesema elimu inatakiwa kuwa jumuishi pamoja na ajira kwa vijana pamoja na Malengo endelevu ya miaka 15 na malengo ya millennia ya miaka 15.
Maadhimisho ya vijana Dunia yalianza yalianzishwa mwaka 1999 katika mkutano mkuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo kauli mbiu mwaka 2019 ni Elimu.