Picha : WFT YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MBINU ZA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA

Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto leo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania limekutana na wadau wa haki za wanawake na watoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Agosti 14,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli na kukutanisha pamoja maafisa wa serikali ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na mkoa,viongozi wa dini,waandishi wa habari,wawakilishi wa baraza la watoto, na asasi za kiraia zinajishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto.


Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia alisema lengo la mkutano huo ni kuwafahamisha wadau wa utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuhusu mradi huo.

"Tumekutana hapa ili kuwafahamisha hatua tuliyofikia katika utekelezaji wa mradi huu ili tuweze kuunganisha jitihada za kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto lakini pia kubaini na kujadili changamoto ambazo wadau wanakutana nazo katika utekelezaji wa MTAKUWWA",alisema Mbia.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu,Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo,Elizabeth Mweyo alisema tayari wameunda kamati za MTAKUWWA katika kata zote 26 na vijiji vyote 126 kati ya hizo kamati tano za ngazi ya kata zimejengewa uwezo.

Alisema kupitia vikundi hivyo wameendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mila na desturi zinazochangia kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuhamasisha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za vikundi.

Nao wadau walioshiriki walizitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii kuwa ni wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili huku wakiwanyooshea vidole baadhi ya Madaktari wasio waaminifu ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kutofika mahakamani kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili wanayopokea.

ANGALIA PICHA  WAKATI WA  MKUTANO
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akielezea lengo la mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto uliofanyika leo katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano huo.


Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Shinyanga ,Elizabeth Mweyo akizungumza katika mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto.

Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini.
Mwakilishi wa BAKWATA Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hemed Rashid akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa  Baraza la watoto kijiji cha Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Stevi Peter Kienze akiomba taarifa za matukio ya ukatili zinapotolewa zifanyiwe kasi haraka ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga ,Lydia Kwesigabo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE ACP, John Myola akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa haki za wanawake na watoto.
Mkutano unaendelea.
Rehema Katabi kutoka shirika la PWWCO akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa kutoka Women Fund Tanzania,Neema Msangi akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mdau kutoka shirika la TAI, Jonathan Kifunda akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mkutano unaendelea.

Wadau wakiwa ukumbini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post