WAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO KWA KATIBU MKUU TAMISEMI


Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amemwagiza Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Joseph Nyamhanga, kuwarejesha mara moja katika kituo cha kazi cha Ipogoro, Manispaa ya Iringa watumishi saba ambao walihamishwa hivi karibuni.

Jafo alitoa agizo hilo jijini Dodoma jana wakati akifungua mkutano wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri.

Alisema kumekuwa na uonevu wa kuwahamisha vituo vya kazi baadhi ya watumishi jambo ambalo linawafanya wapoteze morali ya kazi.

Aidha, Jafo alimwagiza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Zainabu Chaula, kufuatilia kama mganga mkuu wa wilaya ameondolewa kazini kwa haki, kufanya makosa au kuonewa.

“Huyo mganga mkuu wa wilaya, alikuwa anafanya kazi yake kwa moyo, lakini hivi sasa ameondolewa kazini, sasa nataka ufuatilie je ameondolewa kwa makosa yake au nini kimetokea, fuatilia unipe majibu,”alisema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527