WAWEKEZAJI KUTOKA NCHI ZA NJE WAKARIBISHWA KUWEKEZA NCHINI BAADA YA VIKWAZO VILIVYOKUWEPO KUONDOLEWA

NA Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.

Waziri  Mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa amezindua wiki ya uwekezaji KAGERA na mwongozo wa uwekezaji katika mkoa huo kwa kuwaomba wawekezaji kutoka nje ya nchi kuchagamkia fursa zilizoko nchini baada ya vikwazo vilivyokuwepo hapo awali kuondolewa.

Akifungua mwongozo huo Waziri Mkuu amesema kuwa hivi sasa mtu anayetaka kuwekeza nchini anaweza kuanza mchakato akiwa popote kupitia mfumo wa tehama unaowezesha vitu vingi vya uwekezaji kufanyika kwa njia ya mtandao.

Mapema Mkuu wa mkoa  Kagera Brigedia General  Marco Gaguti amesema maeneo makubwa ya uwekezaji yapo katika sekta za kilimo,utalii,ufugaji,uvuvi,viwanda,misitu,madidini na huduma za kijamii.

Wiki ya uwekezaji Kagera iliyoanza  august 12 mwaka huu itahiitimishwa august 17 mwaka huu ambapo shughuli mbalimbali ikiwemo kutambua maeneo ya uwekezaji ,namna ya kuwekeza yanajadaliwa na wadau kuoanga namna ya kuwekeza katika maeneo hayo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post