WALIOSAFIRISHA MADINI YA BILIONI 2 WALIPA FAINI YA MILIONI 341 KUKWEPA KIFUNGO GEREZANI


Madereva wawili na Wafanyabiashara wanne wa Madini ya Dhahahu wamenusurukika kwenda jela miaka 20, baada ya kulipa faini ya zaidi ya Shilingi Milioni 341, baada ya kukiri kosa la kusafirisha la madini ya yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2.


Katika fedha hiyo wa Mil. 341, kiasi cha Sh.Mil 125 ni faini na Sh.Mil 216.5 ni fidia wanayotakiwa kulipa kutokana na kuisababishia Serikali hasara.

Hukumu hiyo imetolewa na  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam, Janeth Mtega baada ya washtakiwa hao kwa ujumla wao kukiri makosa yao na Mahakama ikawatia hatiani na kuwahukumu.

Akiwasomea hukumu hiyo Hakimu Mtega amesema washtakiwa kwa pamoja walishiriki genge la uhalifu, kusafirisha madini nje ya nchi, kuuza madini kinyume na sheria, kushindwa kulipa mrabaha na kuisababishia hasara Serikali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527