Picha : PIKIPIKI YA CCM YAIBIWA SHINYANGA.....POLISI WAKAMATA WAHALIFU 73


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha pikipiki ya CCM iliyoibiwa na kukamatwa na polisi.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kuikamata pikipiki yenye namba za usajili MC 276 BBM aina ya SUNLG Mali ya Chama Cha Mapinduzi ' Umoja wa Wazazi CCM) mkoa wa Shinyanga iliyoibiwa katika ofisi za chama hicho Mjini Shinyanga.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Agosti 18,2019 ,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesema pikipiki hiyo iliibiwa mahali inapohifadhiwa Mjini Shinyanga na jeshi la polisi limefanikiwa kuikamata pikipiki hiyo katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

"Tumeikamata pikipiki hiyo wilayani Bariadi ikiwa imetengenezewa kadi ya kufoji.Tumemkata mtuhumiwa mmoja na tunaendelea kufuatilia kubaini mtandao wa watu wanaotengeneza kadi za kufoji",ameeleza.

Kamanda Abwao amesema pikipiki hiyo ni sehemu ya pikipiki tano ambazo zimekamatwa na polisi kufuatia misako iliyofanywa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia tarehe 23.07.2019 hadi tarehe 18.8.2019 katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.

"Pikipiki hizi zingine tulizozikamata zimetumika katika vitendo vya mauaji ya mwanamke aitwaye Kalekwa Shiku (50) mkazi wa kijiji cha Mishepo,wilaya ya Shinyanga na mauaji ya mwendesha bodaboda Juma Nedadi (28) kisha kuporwa pikipiki yenye namba za usajili MC.841 CCG aina ya Honlg na pikipiki zingine ni zile zilizokuwa zinatumika kusafirishia dawa za kulevya aina ya bangi",alisema Kamanda Abwao.

Alizitaja pikipiki zingine zilizopatikana zinazodhaniwa kuwa ni za wizi kuwa ni zenye namba za usajili T.609 CZE,MC 159 BWQ na MC 881 aina ya SANYA na SANLG.

Alifafanua kuwa katika misako hiyo,Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata watuhumiwa 73 wa uhalifu wakiwemo wa matukio ya mauaji,dawa za kulevya kama vile bangi,wezi,heroine,cocaine na mirungi.


Alisema mbali na kukamata wahalifu pia wamefanikiwa kupata mali zidhaniwazo kuwa ni za wizi ambazo ni pamoja na radio aina ya subwofer,simu tablet,laptop,TV,pikipiki,gari 1(chakavu),betri za gari,solar panel,ng'ombe,booster,baiskeli na madini yyadhaniwayo kuwa ni ya bandia aina ya dhahabu.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao  akielezea kuhusu misako mbalimbali iliyofanywa na jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu leo katika mkutano wake na waandishi wa habari. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Pikipiki ya Umoja wa Wazazi iliyoibiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha pikipiki ya Umoja wa Wazazi CCM iliyoibiwa na kukamatwa na polisi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akielezea namna pikipiki ya Umoja wa Wazazi CCM ilivyoibiwa na kukamatwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha pikipiki zilizoibiwa katika matukio ya mauaji na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.
Pikipiki zilizoibiwa katika matukio ya mauaji na usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao panga lililokuwa linatumiwa na watuhumiwa wa mauaji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha TV Flat inayodhaniwa kuwa ni ya wizi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha laptop aina ya Sumsung inayodhaniwa kuwa ni ya wizi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha kifaa cha kukabia roba kilichokuwa kinatumiwa na wahalifu kuibia watu mali zao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akionesha mifuko iliyobeba bangi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao akiangalia bangi iliyowekewa karanga juu ili mtu akiangalia aone ni mifuko iliyobeba karanga kumbe kuna bangi kwa ndani.

Laptop na vifaa vinavyotumiwa na wahalifu kufanya uhalifu vilivyokamatwa.

Mali za wizi zilizokamatwa na polisi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post