VYAMA 18 NA WAGOMBEA 60 WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 13 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 3, 2019

VYAMA 18 NA WAGOMBEA 60 WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 13

  Malunde       Saturday, August 3, 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliutangazia Umma kuhusu Uchaguzi Mdogowa Udiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 17 Agosti mwaka 2019,kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Na. 292.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, Utoaji wa Fomu za wagombea ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 03 Agosti, 2019 na Uteuzi wa wagombea kufanyi katarehe 03 Agosti, 2019.

Hadi kufikia tarehe 02 Agosti, 2019 saa 10:00 jioni jumla ya wagombea 60 kutoka vyama vya siasa 18 wamechukua fomu za uteuzi.

Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea waliochukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).
Imetolewa leo tarehe 02 Agosti, 2019 na
 Hussein Makame
AFISA HABARI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post