DED KYERWA AWATAKA VIJANA KUWA WABUNIFU,KUTAMBUA VIPAJI VYAO



Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa  Shedrack Mohamed Mhagama

Vijana wilayani Kyerwa mkoani Kagera wametakiwa kuwa wabunifu katika  masuala mbali mbali ya  kiuchumi kuliko kusubiri ajira kutoka serikalini.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 13,2019,na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Shedrack Mohamed Mhagama katika mwendelezo wa wiki ya uwekezaji Kagera yenye lengo la kutangaza fursa za mkoa wa Kagera.

Mhagama amesema vijana wanatakiwa kubuni na kutambua vipaji walivyonavyo kuliko kukaa bila kazi huku baadhi wakisubiri ajira kutoka serikalini.

Mhagama amesema kuwa katika wilaya yake ya Kyerwa kipaumbele ni kwa vijana ili kujenga taifa imara na lenye nguvu.

Amesema vijana wanatakiwa kuchangamkia  fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na halmashauri.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kufanya kazi bila kubagua ili kujikombia kiuchumi kutokana na mkoa wa Kagera kuwa na fursa mbalimbali.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Kagera








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post