HALMASHAURI YA USHETU YAKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 4 KATIKA KIPINDI CHA ROBO YA NNE YA MWAKA 2018/19


 Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeikusanya na kupokea shilingi bilioni 4.5 kutoka serikali kuu kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/19 ambazo zitatumika katika uendeshaji wa halmashauri hiyo.

Akiwasilisha taarifa fedha ya robo ya nne ya mwaka fedha afisa biashara wa halmashauri hiyo, Selestine Lufundisha kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Michael Matomora katika kikao cha kufunga mwaka cha baraza la madiwani amesema mapato ya ndani yaliyokusanywa shilingi milioni 31,001,157,222.61/=

Amesema Halmashauri hiyo imekusanya Mapato ya ndani ambayo ni shilingi 136,871,261.48 sawa na asilimia 58 katika kipindi hicho cha robo ya mwisho wa mwaka wa fedha wa bajeti.

Ameongeza kuwa Fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka robo ya nne ya mwaka ni shilingi milioni 478,068,830 huku shilingi bilioni 3,527,618,500 zikitumika katika ulipaji wa mishara na uendeshaji wa halmashauri.

Amefafanua kuwa Halmashauri hiyo inaendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuhakikisha halmashauri hiyo inaweza kujiendesha pamoja na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao hususani upatikanaji wa huduma za kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha ametoa rai kwa watendaji wa halmashauri hiyo kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato sambamba na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika maeneo yao wanayoishi.

Mbali na hilo Macha ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuitikia kwa vitendo agizo la ununuzi wa vitambulisho vya wajasiriamali ambapo vitambulisho vyote tayari vimeshanunuliwa kwa asilimia 100.
Na Salvatory Ntandu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post