VIONGOZI WA MAANDAMANO YA KUSHINIKIZA NDEGE YA TANZANIA IACHIWE AFRIKA KUSINI WAKAMATWA NA POLISI

Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi walioanzisha maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini wamekamatwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema jeshi la polisi limeyatawanya maandamano hayo kwa kuwa hayana kibali.

Mambosasa amewataka watanzania wawe watulivu kwa kuwa serikali imeshaanza kulishughulikia suala hilo la ndege ya Tanzania inayoshikiliwa Afrika Kusini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post