Picha : MAFUNZO YA KUANDIKA HABARI KIPINDI CHA UCHAGUZI YAFUNGWA MWANZA,…RPC MULIRO ATEMA CHECHEMafunzo ya kuandika habari kipindi cha uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa na Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), chini ya kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC), namna ya kuongeza tija katika kazi za uandishi ili kutoa elimu kwa umma ikiwemo elimu ya uraia na uchaguzi, yamefungwa rasmi leo Jijini Mwanza.


Akizungumza kwenye uhitimishaji wa mafunzo hayo,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Muliro Jumanne Murilo, wakati akiwasilisha mada ya usalama kwa waandishi wa habari, pale wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kuandika habari za uchaguzi, amewataka wanahabari pale wanapokuwa waki ripoti habari kwenye kipindi hicho, wazingatie maadili, Sheria, pamoja na miongozi ambayo hutolewa kwa ajili ya kiusalama, ili wapate kutoa taarifa zao bila ya kubughuziwa.Amesema kwenye kipindi hicho cha uchaguzi kazi ya Jeshi la Polisi hua ni kulinda Amani kwa watu wote wakiwamo na waandishi wa habari, hasa pale wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kuhabarisha umma, lakini inapotokea hofu ya kiusalama hulazimika kuzuia mtu yoyote yule asipite kwenye eneo hatarishi, ndipo msuguano unapoanza kutokea baina ya Jeshi na waandishi wa habari.


“Tatizo ambalo husababisha msuguano kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari, ni pale tunapozuia mtu yeyote yule asipite kwenye eneo la hatari, ndipo wanahabari huanza kutoa vifungu vya kisheria kuwa wana haki ya kutafuta habari, na hatimaye kusababisha kutoelewana,”amesema Muliro.“Mimi ninapo mweka Askari kwenye kituo cha Point “A”au “B” na kutoa agizo (Order), kuwa hakuna mtu yeyote asipite kwenye eneo hilo, ni vyema waandishi wa habari mkatii magizo hayo na siyo kulazimisha kupita tu, ndipo mtabaki kuwa salama na hakutakuwa na msuguano wowote ule baina ya Jeshi na Media, lengo siyo kuzuia habari bali ni kuhakikisha usalama unaendelea kutawala kipindi hicho cha uchaguzi,”ameongeza.


Pia amewataka waandishi wa habari kwenye kipindi hicho cha uchaguzi, waache kufanyakazi kimazoea pamoja na kutanguliza kujuana, bali wafuate misingi, sheria na miongozi ambayo hutolewa, na siyo kulazimisha kufanya kazi kwa madai kila mtu anatekeleza majukumu yake, ndipo kutaondoa misuguano hiyo, na kila mmoja kuwa salama.Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari, kipindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao wawe na vifaa kamili vya kazi, vikiwamo na vya kiusalama, kuwa na vitambulisho vya vyombo vyao vya habari, pamoja na kuvaa makoti yaliyoandikwa PRESS, ili wapate kutambulika wakati wa kutafuta habari na kutobughuziwa na mtu yoyote yule.

Naye Mwezeshaji Gasirigwa Sengiyumva ambaye ni mkurugenzi wa taasisi wa vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA), amewataka waandishi wa habari pindi wanapoandika taarifa zao kwenye kipindi hiki cha uchaguzi, wazingatie maadili pamoja na miiko ya taaluma yao ili wapate kutoa taarifa sahihi kwa umma.Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo, wameupongeza mtandao huo wa asasi wa kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), kwa kutoa mafunzo ambayo yatawasaidia kuandika habari kwa ufasaha za uchaguzi, pamoja na kuwa habarisha umma taarifa sahihi.Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, Kigoma, Kagera, Mara, pamoja na Mwanza, ambayo yamedumu kwa muda wa siku tatu kuanzia Agost 22 hadi 24 kwenye ukumbi wa mikutano wa Belmont Hotel Jijini Mwanza.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Muliro  Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi, na kuwataka wazingatie, maadili, miiko ya taaluma yao, pamoja na miongozo ambayo hutolewa wakati wakitekeleza majukumu yao kipindi cha uchaguzi ili wapate kuwa salama.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Muliro Jumanne Muliro , akiwaeleza waandishi wa habari kuwa usalama wao wakati wa kuandika habari kipindi cha uchaguzi upo mikononi mwao kwa asilimia 70, endapo wakiti miongozo, Sheria, maadili, maagizo ambayo hutolewa, kuwa na vifaa vya kazi, yakiwamo mavazi ya kiusalama, pamoja na kuvaa vitambulisho na makoti yaliyoandikwa PRESS.

Mwezeshaji Gasirigwa Sengiyumva ambaye ni mkurugenzi wa taasisi wa vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA),akiwataka waandishi wa habari pindi wanapokuwa wakiandika habari za uchaguzi wazingatie maadili ya taaluma yao, ili wawe wanatoa taarifa sahihi za kuhabarisha umma.

Mwezeshaji Dastani Kamanzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ujuzi Era, akiwataka waandishi wa habari pia wawe wabobezi wa kuandika habari ya mlengo mmoja(Specialized) mfano habari za afya tu, kilimo, uchumi, na siyo kuwa waandishi wa kuandika kila habari.

Mwandishi wa habari Ester Sumira kutoka Azam Tv Mkoani Geita akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Paulina David kutoka Radio Free Afrika Jijini Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi Salma Mrisho kutoka Star Tv Mkoani Geita, akichangia mada kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi yaliyofanyika Jijini Mwanza.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.


Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi.

Mratibu wa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi Joseph Moses Oleshaghai kutoka kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC), amesema wametoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, wakiamini kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu wa kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya kiraia na uchaguzi.


Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali , wakiwa na wawezeshaji wa mafunzo ya kuandika habari za uchaguzi, wakipiga picha ya pamoja na Kamanda ya Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Murilo Jumanne Murilo mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo yaliyodumu ndani ya siku Tatu kuanzia Agost 22 hadi 24 kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Belmont Jijini Mwanza.


Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post