Picha : TACCEO YAENDESHA MAFUNZO YA UCHAGUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA



Mwezeshaji kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za uchaguzi wakili wa kutoka kampuni ya TIFLD Gelina Fuko akizungumza kwenye mafunzo hayo. 


Na Marco Maduhu - Malunde1 blog


Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia uchaguzi Tanzania (TACCEO), chini ya kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC), umeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari Kanda ya Ziwa wakikusudia kuongeza tija katika kazi za uandishi ili kutoa elimu kwa umma ikiwemo elimu ya uchaguzi.

Mafunzo hayo yameanza leo Alhamsi Agosti 22,2019 ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu hadi Agost 24,2019  katika ukumbi wa mikutano Belmont Hotel Jijini Mwanza, yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu, Geita, Mara, Kagera, Kigoma na Mwanza.


Mratibu wa mafunzo hayo, Joseph Moses Oleshaghai kutoka kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC), amesema wanatoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari, wakiamini kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu wa kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya kiraia na uchaguzi.


“Tunatoa mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuwaongezea tija kwenye kuandika habari za uchaguzi na kuwapatia wananchi ujumbe sahihi, ambao una husu masuala ya elimu ya uraia na uchaguzi, pamoja na kuwa hamasisha kujitokeza kugombea uongozi, kujiandikisha, pamoja na kupiga kura,”amesema Oleshaghai.


Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo wakili kutoka Kampuni ya (TIFLD) Jijini Dar es salaam Gelina Fuko, amewataka waandishi wa habari pale wanapokuwa wakiandika habari zao kwenye kipindi hiki cha uchaguzi, wazingatie kupaza sauti za makundi mbalimbali wakiwamo watu wenye uhitaji, walemavu, wanawake, na wazee ili waweze kupata haki zao kwenye uchaguzi.


Amesema kwenye kipindi cha uchaguzi makundi hayo maalumu ya mekuwa yakisahaurika kupaziwa sauti, na hivyo kuendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye uchaguzi, ikiwamo kunyimwa haki ya kugombea, kubaguliwa, ambapo msaada wao ni waandishi wa habari.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mratibu wa mafunzo ya habari za uchaguzi kwa waandishi wa habari Joseph Moses Oleshaghai kutoka kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC),akielezea dhumuni wa mafunzo kuhusu masuala ya uchaguzi kwa waandishi wa habari wa Kanda ya Ziwa leo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mwezeshaji kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za uchaguzi wakili wa kutoka kampuni ya Tangible Initiatives for Local Development Tanzania (TIFLD) Gelina Fuko, akiwataka wanahabari kupaza pia sauti za watu wenye uhitaji kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ili waweze kupata haki zao.

Mwandishi wa habari Nashoni Kenedy kutoka Gazeti la Daily News Jijini Mwanza, akichangia mada kwenye mafunzo hayo ya wanahabari jinsi ya kuandika habari za uchaguzi na kuhabarisha umma kupitia vyombo vyao vya habari.

Mwandishi wa habari Moshi Ndugulile kutoka Radio Faraja Mkoani Shinyanga ,akichangia mada kwenye mafunzo hayo ya wanahabari Kanda ya Ziwa juu ya kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi na kuhabarisha umma kupitia vyombo vyao vya habari.

Mwandishi wa habari Salma Mrisho kutoka STARTV Mkoani Geita, akichangia mada kwenye mafunzo hayo ya wanahabari Kanda ya Ziwa juu ya kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma yao na kutokwenda kinyume na sheria za uchaguzi.

Mwandishi wa habari za mitandaoni Fedrick Chibuga kutoka BMG Online TV Jijini Mwanza, akichangia mada kwenye mafunzo hayo ya wana habari kutoka Kanda ya Ziwa juu ya kuandika habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari za mitandaoni Salvatory Ntandu kutoka Mpekuzi Blog, akichangia mada kwenye mafunzo hayo ya wanahabari kutoka Kanda ya Ziwa namna ya kuandika kwa usahihi habari za uchaguzi.

Mwandishi wa habari Joel Maduka kutoka Radio Storm FM Mkoani Geita naye akichangia mada kwenye mafunzo hayo wana habari Kanda ya ziwa namna ya kuandika habari sahihi za uchaguzi na kutoa elimu ya uraia na uchaguzi kwa wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo Jijini Mwanza namna ya kuandika habari sahihi za uchaguzi, pamoja na kutumia vyombo vyao kutoa elimu ya uraia na uchaguzi kwa wananchi.

Mafunzo yakiendelea namna ya kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na sheria za uchaguzi.

Mafunzo yakiendelea namna ya kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na sheria za uchaguzi na kuhabarisha umma kupitia vyombo vyao vya habari.

Mafunzo yakiendelea namna ya kuandika habari za uchaguzi kwa usahihi pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na sheria za uchaguzi.

Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo Jijini Mwanza  namna ya kuandika habari sahihi za uchaguzi, pamoja na kutumia vyombo  vyao kutoa elimu ya uraia na uchaguzi kwa wananchi.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post