ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUFANYA KAZI NA SERIKALI KUHUDUMIA JAMII


Mkufunzi  kutoka  THRDC  wakili Deo  Bwire  akitoa  mafunzo kwa  washiriki  wa  mafunzo  kutoka asasi za   kiraia  mkoa wa Njombe na Iringa jana

Na Francis Godwin,Iringa 
Wito  umetolewa kwa mashirika ya utetezi wa haki za binadamu nchini kuendelea kufanya kazi ya kuisaidia serikali katika masuala mbali mbali ya kijamii kama afya,elimu na mengine ambayo ambayo serikali imekuwa ikifanya.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka asasi za kiraia kanda ya nyanda za juu kutoka mkoa wa Njombe na Iringa jana . mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC), wakili Deogratias Bwire.

Alisema  ipo dhana potofu kwa jamii juu ya kazi za watetezi wa haki za binadamu kwa kumuona mtetezi kama ni mchochezi jambo ambalo si sahihi kwani mtetezi ni mtu yeyote anayefanya kazi ya kusaidia kuokoa maisha ya mwingine.

Alisema kuwa mwaka 1998 baraza kuu la umoja wa mataifa lilidhia azimio la haki za binadamu japo kwa vipindi tofauti tofauti matamko mbali mbali yalitolewa na hadi nchi mbali mbali ziliweza kuja na sera ya haki ya binadamu japo kwa Tanzania bado hatujawa na sheria ama sera ya kuwatambua watetezi.

Alisema matamko ambayo yamepata kutolewa kikanda ni kama tamko la Grad Bay la mwaka 1999 ,tamko la Kigali la mwaka 2003 ,makubaliano 2004 (Mwakilishi wa watetezi) , mpango wa kikazi wa Kampala ( KAPA 2009) huku kitaifa ni THRDC (makubaliano ya Newafrica Hotel).

“Nani mwenye jukumu kumlinda mtetezi ,azimio la watetezi wa Haki za binadamu linasisitiza kwamba nchi ndiyo ya kwanza katika kuwalinda watetezi wa Haki za binadamu",alihoji Bwire.

Aidha alisema kuwa makundi na miungano inayochangia katika kuboresha ukiukaji wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi hivyo basi ukiangalia ibara ya 12 ya tamko hiloinatamka wazi kwamba dola ina mamlaka ya kumlinda mtetezi wa haki za binadamu.

Alizitaja haki za mtetezi kuwa ni kulinda na kustawisha haki za binadamu ,kulindwa , kuchunguza na kupata habari ,kutoa maoni ,kukusanyika kwa amani ,kuunda asasi na kupata fedha za miradi pamoja na kuweza kuifikia mahakama.

Bwire alisema kuwa watetezi wa haki za binadamu wanatambulika kote duniani na serikali inajukumu la kuwalinda watetezi ,lakini sote tuna jukumu hilo na THRDC ni mtandao kwa ajili ya watetezi.

Hivyo alisema kuwa mafunzo ya utetezi wa Kimkakati na usalama kwa Watetezi wanaofanya kazi za utetezi wa haki za Kijamii kwa mikoa ya Iringa na Njombe ambayo yameandaliwa na THRDC ni kuweza kuwajengea uwezo zaidi ili kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

“Haki za Kijamii zitakazofundishwa zinahusisha haki za elimu bora, afya bora, chakula, maji safi, malazi yenye staha na haki za hifadhi ya jamii (social security) pamoja na mambo mengine”, alisema.

Alisema watetezi hao watajengewa uwezo juu ya mabadiliko ya 2019 ya sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikari ya mwaka 2002 na kuelekezwa namna bora ya kufuata sheria za Mashirika yasiyo ya kiserikali na sheria nyingine za nchi kama njia mojawapo ya kuhakikisha usalama wa Mashirika hayo.

Wakitoa maoni yao katika mafunzon hayo washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa wengi wao wamekuwa wakifanya kazi ya utetezi bila kujua wao wanafanya kazi ngani na wakati mwingine wanakuwa katika mazingira magumu pasipo kujua nani wa kumtetea.

Aliwataka watetezi hao kutoogopa sheria zilizotungwa badala yake kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi huku wakitambua sheria na mazingira ya kazi ya utetezi.

Hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi wanaweza kupiga hatua ya kuboresha kazi zao na hata kuisaidia jamii na serikali katika uwajibikaji wake wa kila siku wenye lengo la kusaidiana pamoja kuhudumia jamii.
Mkufunzi kutoka THRDC wakili Deo Bwire akitoa mafunzo kwa washiriki wa mafunzo kutoka asasi za kiraia mkoa wa Njombe na Iringa jana
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia masomo
Washiriki wakiwa darasani kuendelea na mafunzo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527