TANGA UWASA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA WAZIRI UMMY WAMKABIDHI SARUJI NA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI TATU JIJINI TANGA”


 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katika akikata utepe kuashiria kupokea  Msaada wa madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20 kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4 uliotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge

 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kupokea  Msaada wa madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20  kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4  kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi madawati madawati 20 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mhandisi Geofrey Hilly
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi madawati hayo pia Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange kushoto mara baada ya kuyapokea kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa kushoto Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa  Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu kushoto ni  Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange
 Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge akizungumza wakati wa halfa hiyo
  Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge  akizungumza wakati wa halfa hiyo
 Afisa Habari Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange akizungumza
 Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
 Sehemu ya wananchi ambao wamehudhuria kwenye halfa hiyo
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM)  Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly mara baada ya kuwasili
 Sehemu ya madawati yaliyokabidhiwa
 Sehemu ya wanafunzi kwenye shule hiyo


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) leo wamekabidhi msaada wa samani na vifaa vya ujenzi kwa shule za msingi Kiruku ,Kibafuta na Pande zilizopo kata za Mabokweni na Kiomono kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Msaada huo ni madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20 kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4 ikiwa ni juhudi za Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu.

Juhudi hizo zinatokana na shule hizo kukabiliwa na upungufu huo hali iliyomlazimu Waziri Ummy kupeleka maombi yake kwenye uongozi wa Tanga Uwasa ambao waliridhia kumsaidia na kuweza kufanikisha vitu hivyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ummy aliioshukuru Tanga Uwasa kwa msaada huo ambao utasaidia kuondosha changamoto zilizopo kwenye shule hizo ili kutoa fursa wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote.

“Niwashukuru sana Tanga Uwasa kwa msaada huu ambao mmetupatia niwaambie kwamba nyie ni taasisi ya serikali inayofanya vizuri zaidi Tanzania kuliko yoyote hivyo tutaendelea kushirikiana “Alisema.

Aidha pia Waziri huyo alizungumzia afya ya msingi mkubwa wa afya ni lishe huku akieleza kwamba kuna tatizo kubwa la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Alisema kwamba tatizo hilo ni kubwa sana nchini ambapo kila watoto 100 watoto 31 wana udumavu maana yake wana utapiamlo uliopitiliza moja ya kupambana nao ni kuhakikisha watoto wanapata lishe bora. 

“labda nihaidi kwamba akupitia Taasisi yangu ya Tawode shamba la ekari tatu lililopo hapa shuleni tutalilima na kupanda viazi lishe wanafunzi waweze kupata chakula wakati wa masomo yao”Alisema

“Kwa hiyo mwalimu mkuu tukutane atakumtanisha na mtendaji wao wa tawode wapande viazi lishe anaiteba kwa sababu hauwezi kubeba kujenga Tanzania ya viwanda kama watoto milioni 3 kati ya watoto milioni 9 wenye umri chini ya miaka mitano Tanzania wana udumavu “Alisema

“Kwa sababu ni asilimia 31 ni watoto milioni 3 walimu watafundisha lakini watoto watakuwa wamedumaa na watakuwa hawaelewi hivyo nitakwenda kuhakikisha anakuja mratibu wetu hapa kuweza kushirikiana nanyi.

Awali akizungumza wakati mara baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba mchango huo ni muendelezo wa mpango wa mamlaka hiyo kuchangia sekta ya elimu kwa kuangalia maeneo yenye mahitaji. 

“Tulifahamu Kiruku na shule hizo nyengine walikuwa wana mahitaji hayo ndio maana wameamua kuchangia tunamshukuru Waziri Ummy na mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa alipeleka ombi hilo mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Tanga Uwasa na wao wakaamua kuunga mkono juhudi hizo mkono juhudi zikiwemo za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ya kutoa elimu bure.

Aidha alisema kwamba wanategemea vifaa hivyo vitatumika kwa uangalifu mzuri na kwa malengo yaliyokusuiwa na darasa liweze kukamilika huku akishukuru ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiupata ikiwemo kuhamasisha wanafunzi wa shule hizo kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu ya maji na mazingira katika maisha yao na huku mbele watapata wataalamu wengi.

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge alishukuru kwa msaada huo huku akieleza kwamba shule hiyo ilikuwa na changamoto wanahitaji madarasa mawili kutokana na kwamba yaliyopo ni chakavu na yana mashimo na mengine hayana sakafu.

Alisema pia shule hiyo ina kabiliwa na changamoto ya kutokuwa na maji ya kisima wala bomba wala tenki lolote hivyo wanaomba wasaidiwe japo kuchimbwa kisima huku ekieleza kwamba pia ofisi ya walimu hawana viti ni chakavu na masheflu ya kuhifadhia vifaa vya shule hayapo kwenye ubora unaotakiwa.

“Mh Waziri mahitaji ya madawati awali tulikuwa tunahitaji madawati 20 yaliyokuwepo madawati 127 pungufu ni 20 baada ya kupokea madawati hayo hatutakuwa na mapungufu tena hivyo kunakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa tunakuomba mungu akuzidishie”Alisema

Hata hivyo kwa wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Khalifa Shemahonge ambaye pia ni Afisa elimu Msingi Jiji la Tanga alisema wao wana Tanga wanapomuona mahali popote Tanzania Waziri Ummy wanajisikia farahi kutokana na kwamba kuna vitu ametafsiri kwa vitendo maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuongeza pale serikali imeishia yeye binafsi kwa nafasi yake

“Nakumbuka uliniita na kuniambia niandike andiko la shule zenye upungufu nikaombe fedha nikafanya hivyo na andiko hilo lilileta tija kubwa ya uyjenzi wa madarasa nikushukuru sana Waziri Ummy kwani umekuwa msaada mkubwa sana kwetu “Alisema 

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange alisema kwamba wanasimama kwa kumshuru Mungu lakini kwa juhudi unazofanya kwenye Jiji la Tanga kusaidia sekta ya elimu umekuwa mtu mzuri kwa sababu unakumbuka kwenu,kwa sisi Tanga ww ni mama yetu kwa kila kitu,nakumbuka tulikuwa na tatizo la ongezeko la ufaulu ulisimama kidete na kujengwa vyumba vitano vya madarasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post