TETESI ZA SOKA LEO ALHAMIS AGOSTI 29,2019


Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)

Barcelona na Paris St-Germain zimekubali malipo ya uhamisho wa mchezaji wa miaka 27 wa timu ya taifa ya Brazil Neymar, lakini majadiliano yanaendelea kuhusu makubaliano ya mkataba huo. PSG inataka mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ufaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 22, kuwa sehemu ya mpangilio huo. (Mirror)

Hatahivyo, Ajenti wa Dembele anasema mchezaji huyo hatoondoka Nou Camp, hatua ambayo huenda ikachangia kupromoka kwa pendekezo la uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona. (Daily Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, mwenye umri wa miaka 25, amekubali makubaliano ya kujiunga upya na Monaco kwa mkopo - huku kukipangiwa malipo ya £31.8m ka mkataba wa kudumu.(RMC Sport, kupitia Sun)
Mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal, mwenye umri wa miaka 33, c huenda akarudi katika klabu alikotoka Uhispania kaba ya kufungwa dirisha la uhamisho Ulaya Jumatatu, huku Real Sociedad ikiwa na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Osasuna na Malaga. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya England Sam Greenwood, mwenye umri wa miaka 17, ametambuliwa na timu bingwa ya Italia AC Milan na Juventus kama mchezaji anayelengwa baada ya kuridhisha maajenti katika mshindano ya ubingwa wa Ulaya wa timu za wachezaji walio chini ya umri wamiaka 17 mapema msimu huu wa joto. (Sun)

Manchester United italipa kitita cha £300,000 cha malipo ya Alexis Sanchez ya £400,000 kwa wiki wakatimchezaji huyo wa kiiungo cha mbele wa Chile akiwa uhamishoni kwa mkopo huko Inter Milan. (Metro)Alexis Sanchez alijiunga na Manchester United mnamo Januari 2018

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa RB Leipzig na anayelengwa na Liverpool, Timo Werner, mwenye umri wa miaka 23, bado hajakata tamaa ya uhamisho kwenda ng'ambo katika siku za usoni licha ya mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Ujerumani kusaini mktaba mpya katika klabu hiyo kwenye ligi ya Bundesliga. (Mirror)

Kipa wa Bournemouth Asmir Begovic, mwenye umri wa miaka 32, huenda akaondoka baada ya kuipoteza nafasi yake kwa mchezaji wamiaka 21 wa England Aaron Ramsdale. (Sun)

Mshambuliaji wa Reading Sam Baldock, mwenye umri wa miaka 30, anavutia vilabu kadhaa katika ligi ya Ujerumani Bundesliga 2, huku mlinzi mwenye miaka 19 wa timu ya taifa ya England Tom Holmes akitarajiwa kujiunga na KSV Roeselare huko Ubelgiji kwa mkopo. (Get Reading)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City Giannelli Imbula, mwenye miaka 26, anakaribia kuhamia kwa mkopo kwenda klabu katika ligi ya Serie A. (Sport Italia)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionChristian Eriksen

Tottenham hawana uhakika na nia ya Christian Eriksen kutokana na kuvunjika kwa mahusiano kati ya mwenyekiti wao Daniel Levy na wakala wa kiungo huyo mwenye miaka 27 raia wa Denmark. (Guardian)

Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Eriksen anatakiwa kuanza kwenye mechi za Spurs licha ya kutokujulikana kwa hatma yake ya mbeleni. (Talksport)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 26 aliondoka Manchester United kwa sababu alichoshwa na klabu hiyo , kwa mujibu wa kocha wa Belgium Roberto Martinez. (Mirror).

Kaka yake Paul Pogba, Mathias mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Deportivo Manchego, amesema mdogo wake anayechezea Manchester United itapendeza zaidi kama atahamia Real Madrid. (AS)
Mshambuliaji wa Everton Cenk Tosun anataka kubaki katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ana mpango wa kuhamia Eintracht Frankfurt. (Turkish Football)

Liverpool imesema kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake Bobby Duncan na imekataa kutumia mbinu za Fiorentina. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa Brighton, Jurgen Locadia, 25 anaweza kusajiliwa kwa mkopo na Bundesliga side Hoffenheim. (Argus)

Olympiakos wako katika mazungumzo na klabu ya Leicester katika mpango mpya wa kumsajili mshambuliaji wa Foxes ambaye ni raia wa Algeria Rachid Ghezzal, 27. (Sky Sports)

Manchester City wapo katika mipango ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Hearts Aaron Hickey kwa dau la paundi milioni 1.5 ili kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ifikapo mwezi Januari. (Sun)

Kiungo wa klabu ya West Bromwich Albion, Rekeem Harper mwenye umri wa miaka 19 amepewa nafasi kubwa katika mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo Slaven Bilic katika msimu huu. (Express and Star)
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post