RPC MOROGORO KASEMA ZAIDI YA WATU 57 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA LORI LILILOWAKA MOTO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi August 10, 2019  umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa , baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza  kujazana  wakigombania kuchota mafuta ambapo mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alianza kuvuta betri ya gari na ikawa ndo chanzo cha moto kulipuka


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527