RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU NA JOÃO MANUEL GONÇALVES LOURENÇO WA ANGOLA WAWASILI NCHINI TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA SADC


Marais wawili, Edgar Lungu wa Zambia na João Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola wamewasili Tanzania kuhudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mkutano huo unaoshirikisha nchi 16 za SADC unafanyika kuanzia kesho Jumamosi jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais John Magufuli wa Tanzania.

Marais wengine waliokwisha kuwasili nchini ni; Danny Faure wa Shelisheli na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527