RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI KUTUA DAR JUMATANO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 12, 2019

RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI KUTUA DAR JUMATANO

  Malunde       Monday, August 12, 2019

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosa atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wa wakuu  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia Agosti 16, ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post