RAIS MAGUFULI KUZINDUA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TERMINAL 3 LEO


Rais John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019, anatarajia kuzindua mradi wa upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere la terminal 3, ambao umetekelezwa kwa miaka6 kwa gharama ya Sh788.6 bilioni.

Mradi huo ulianza kujengwa 2013 na awali ulipangwa kutekelezwa kwa Sh705.3 bilioni lakini kutokana na kubadilika kwa taratibu za kikodi, mchoro wa mradi (Design) na gharama ya mradi huo iliongezeka kwa Sh85.3 bilioni.

Wakati mradi unaanza ulitarajiwa kuwa ungekamilika Desemba 2017, baadaye ukaongezewa mwaka mmoja hadi Desemba 2018, lakini haukukamilika badala yake umekamilika Mei, mwaka huu.

Kampuni iliyotekeleza mradi huo ni BAM International ya Uholanzi ambayo ndiyo iliyofanya kazi za kikandarasi na Arab Consulting Engineers (ACE) ya Misri, ilifanya kazi za ushauri.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527