RAIS MAGUFULI ATAKA KUFUTWA UTITIRI WA KODI SADC


Rais   Magufuli amehimiza sekta binafsi katika nchi za SADC kuendelea kuwa na ujasiri wa kufungua viwanda vingi hapa nchini kwa kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira  mazuri ya uwekezaji.

Rais Dkt.Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua Maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi  za SADC jijini Dar Es Salaam na kusisitiza umuhimu wa kufungua viwanda vingi wakati huu mazingira ya uwekezaji yakiboreshwa ikiwemo ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji utakaosaidia kupunguza bei ya umeme pindi utakapokamilika.

Katika hotuba yake ya ufunguza Rais Dkt.Magufuli amendelea kuhimiza umuhimu wa kufutwa kwa utitiri mkubwa wa kodi kwa nchi za wanachama wa SADC kwa lengo la kuongeza hamasa ya uwekezaji wa viwanda vitavyosaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi kwa nchi za SADC.

Kadhalika Rais Dkt.Magufuli amehimiza uwekezaji pia katika viwanda vya madini kwa kuwa nchi nyingi za SADC zina rasilimali za kutosha za madini na kupongeza uwekezaji wa viwanda hapa  inayofikisha viwanda elfu nne kwa sasa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527