RAIS MAGUFULI APIGA ‘PUSH-UP’ TENA DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga Push Up na wasanii wa Tanzania One Theatre (TOT) wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Agosti 1, 2019.

Rais  wa Tanzania, John Magufuli leo Alhamisi Agosti Mosi, 2019 amepiga ‘push-up’ tisa kabla ya kuzindua jengo jipya la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).



Katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, ilikuwa ni kawaida kumshuhudia Rais Magufuli akipiga ‘push-up’ katika mikutano yake mbalimbali hali iliyotafsiriwa kuwa yuko imara kuwatumikia Watanzania.

Leo amerudia tena wakati akiongoza viongozi walioketi meza kuu kwenda kuwatunza waimbaji wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).

Alipofika mbele ya wanenguaji wa bendi hiyo alisimama mbele yao kupiga  ‘push-up’ tisa na kunyanyuka hali iliyoibua shangwe kwa waliohudhuria uzinduzi huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527