MAKONDA AIBUKA NA MKAKATI MWINGINE ...."PEKENYUA TUKUFUKUNYUE" | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 29, 2019

MAKONDA AIBUKA NA MKAKATI MWINGINE ...."PEKENYUA TUKUFUKUNYUE"

  Malunde       Thursday, August 29, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Agosti 29,2019 amezindua Mpango Mkakati wa Kutokomeza  Wahamihaji haramu Mkoa wa Dar es salaam alioubatiza jina la  "PEKENYUA TUKUFUKUNYUE" na  kuwaagiza Watendaji wa Mitaa kurejesha Daftari la Mkazi ili Kila Mkazi kuanzia ngazi ya Mtaa afahamike anapoishi na kazi anayofanya jambo litakalosaidia pia kuondoa uhalifu.


Makonda amesema mpango huo ni Mwarobaini tosha wa kupambana na Wageni wanaoishi Nchini kinyume na Sheria na utahusisha Watendaji wa Kata, Mitaa na Wananchi ambao watakuwa na jukumu la kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa mgeni au mtu wanaemtilia mashaka kwenye Makazi wanayoishi.

Aidha Makonda amesema uwepo wa Wahamihaji Haramu Nchini ni jambo la hatari kiusalama kwakuwa baadhi yao wanafanya uhalifu wa Wizi, Ubakaji, Uporaji, wanatumia rasilimali za nchi, wanatumia fursa ambazo zilipaswa kuwanufaisha wazawa ikiwemo Afya, Elimu na Ajira, kusababisha msogamano wa watu magerezani pamoja na kuwa Chanzo cha Migogo ikiwemo ya Ardhi.

Kutokana na hilo Makonda ameviagiza Vyombo Vyote vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Viongozi wa Kata na Mitaa kuhakikisha Mpango huo unafanikiwa kwa 100%.

Kwa upande wake Kamishina wa Uhamihaji Mkoa wa Dar es salaam amesema wamebaini idadi kubwa ya wahamihaji haramu wanatoka mataifa ya Burundi, DRC, Somalia na Ethiopia na wamekuwa wakipendelea kuishi Mkoa wa Dar es salaam kwakuwa umekuwa jiji lenye fursa nyingi za kibiashara.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post