NDEGE YAANGUKA NA KUUA WATU WAWILI WILAYANI SIKONGE | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 4, 2019

NDEGE YAANGUKA NA KUUA WATU WAWILI WILAYANI SIKONGE

  Malunde       Sunday, August 4, 2019
NA EVELINA ODEMBA-OFISI YA DED SIKONGE

WATU wawili raia wa Afrika Kusini wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea mapema asubuhi ya leo majira ya saa moja na nusu katika kata ya Igigwa Wilayani Sikonge.

Watu hao waliotambulika kwa majina ya D. Werner mwenye umri wa miaka hamsini na nane 58 pamoja na Werner Fredrick Fronaman mwenye umri wa miaka 36 wote wanamme na raia wa Durbun Afrika ya kusini walikuwa kwenye ndege yenye namba za usajili 19-ZU-TAF mali ya Afrika Kusini.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo na kusema kuwa watu hao  walikuwa katika ziara ya kuhamasisha wanafunzi barani Afrika kusomea maswala ya Anga.

Kabla ya ajali kutokea Ijumaa walitua kwa dharula katika uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Entebe Uganda kuelekea Lilongwe Malawi ili kufika Afrika ya kusini. 

Jana asubuhi walipoanza safari, baada ya muda mchache walifanya mawasiliano na wataalamu wa uwanja wa ndege wa Tabora na kutoa taarifa kuwa injini ya ndege imezimika ghafla wakiwa angani hivyo wanafanya utaratibu wa kurudi Tabora.

Baada ya taarifa hizo hawakuweza kupatikana mpaka walipopata taarifa ya ajali hiyo na kufika wakakuta raia hao wameshafariki.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post