MWANDISHI ERICK KABENDERA ARUDISHWA RUMANDE HADI AGOSTI 30

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera bado haujakamilika.


Simon ameeleza hayo leo Jumatatu Agosti 19, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustina Mmbando

Mbali na upelelezi kutokamilika, Pia, hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Augustine Rwizile amepata udhuru.

Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi kiasi cha Tsh. Milioni 173,247,047.02, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu Makosa ambayo  hayana dhamana

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2019 itakapotajwa tena.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527