MBUNGE YOSEPHER KUFIKISHA KILIO CHA WANANCHI WA KIJIJI CHA UPARE WIZARA YA AFYA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 3, 2019

MBUNGE YOSEPHER KUFIKISHA KILIO CHA WANANCHI WA KIJIJI CHA UPARE WIZARA YA AFYA

  TANGA RAHA BLOG       Saturday, August 3, 2019
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua.

 Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba kushoto akichukua kero za wananchi  wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge huyo
  Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba  kushoto akisalimiana na wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao wakati wa ziara yake
UKOSEFU wa Huduma za Afya kwenye Kijiji cha Upare Kitongoji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga kumepelekea Mbunge wa Viti Maalumu mkoa huo (Chadema) Yosepher Komba kujitwisha mzigo huo na sasa anakusudia kwenda Wizara ya Afya ili kufikisha kilio hicho.

Hatua ya Mbunge huyo inatokana na kilio cha wananchi hao ambao walieleza kwamba idadi yao ni wakazi zaidi ya 600 wakati wa ziara yake wakieleza tatizo la kukosa zahanati na kulazimika kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Teule.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kusikiliza kilio hicho alisema kwamba sheria ya Wizara ya Afya kila Kijiji kinapaswa kuwa na Zahanati hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha kijiji hicho kinapatiwa huduma ya afya ili kuweza kunusuru afya za wananchi wa maeneo hayo hasa kinamama na watoto.

Mbunge huyo alisema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo atakwenda kukutana na Waziri Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ili kumueleza tatizo hilo kwani haiwezekani zaidi ya wananchi 600 katika kijiji hiki wanakosa huduma ya afya hii ni hatari kwa ustawa wa afya zao.

Alisema anashangazwa na viongozi wa Serikali wanaofanya ziara katika maeneo mbalimbali ya wilaya na wanajua tatizo hilo la kutokuwepo kwa huduma hiyo ya afya huku hakuna hatua zozote ziznazochukuliwa ili kuwasaidia wananchi hao.

Alisema ni jukumu la viongozi kutenda haki katika nyanja zote ili kutenda usawa wa huduma za kijamii na kuweka mazingira rafiki ya afya kwa wananchi hao kuliko kusubiria athari zitokee na kuanza kutafuta chanzo.

Awali wakizungumzia hali wananchi wa maeneo hayo alisema wanalazimika kutembea zaidi ya km 12 kuelekea Wilayani Muheza kupata huduma bora ya afya jambo ambalo linahatarisha maisha yao.

Mmoja wa wananchi hao Frednand Francis alisema ipo haja kwa Serikali kupitia Wizara yake kuwahurumia wananchi hao katika suala zima la afya ambayo ndio msingi wa maisha ya mwanadamu.

Francis alisema ni kitu cha ajabu kuona kijiji hicho kilichokuwa na wakazi zaidi ya 600 huku kikosa huduma hiyo ya afya jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao na watoto ambao ndio msingi wa Taifa lijalo.

Hata hivyo alimuomba kuwasaidia kufikisha kilio hicho kwa Waziri mwenye dhama juu ya hali mbaya kukosa huduma ya afya jambo ambalo ambalo linaweza kuleta madhara baadae kutokana na wananchi wengi kuathirika na maradhi.

Mwisho.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post