MBUNGE BOBI WINE WA UGANDA ASHTAKIWA KWA KUMKASIRISHA RAIS YOWERI MUSEVENI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 7, 2019

MBUNGE BOBI WINE WA UGANDA ASHTAKIWA KWA KUMKASIRISHA RAIS YOWERI MUSEVENI

  Malunde       Wednesday, August 7, 2019

Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye ni mashuhuri zaidi kwa jina la Bobi Wine ameshtakiwa kwa kosa la kumkasirisha na kumkejeli Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Mbunge huyo na wenzake wanatuhumiwa pia kuurushia mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini wa Arua mwaka uliopita wa 2018.

 Aidha shitaka hilo jipya limeongezwa katika orodha ya mashtaka mengine yanayomkabili Mbunge huyo wa upinzani likiwemo lile la uhaini. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa, iwapo Bobi Wine atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Bobi Wine bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyingine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za mkononi.

Halikadhalika, Mbunge hivi karibuni alitangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post