MADEREVA WA DALADALA DODOMA WAGOMA KISA MACHINGA KUZAGAA STENDI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Madereva  Wa  Daladala katika kituo cha daladala  sabasaba  jijini Dodoma  wamegoma kufanya safari wakishinikiza wamachinga kuondolewa kutokana na ufinyo wa nafasi katika eneo hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari hapo jana Agosti 19,2019  baadhi ya madereva wamesema kuwa,wamegoma kutokana na machinga kutokuwa na utaratibu mzuri wa kufanya biashara.

Baadhi ya abiria waliokuwa wakifanaya safari zao za kutoka na kuingia ndani ya stand hiyo wanaeleza athari za mgomo huo,kama anavyoeleza Franco James wakiwa na wenzake.

Akizungumza na madereva hao mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi mbali na kuomba madereva hao kuendelea kusafirisha, amepiga marufuku baadhi ya biashara ikiwemo uchomaji mshikaki .

Mgomo huo Ulimalizika na shughuli zikaendelea kama kawaida katika kituo cha daladala cha SABASABA jijini  Dodoma baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuingilia kati na kuamru wafanyabiashara hususan wakaanga mishikaki kutofanyia biashara katika kituo hicho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post