KUNDI LA WAASI LA HOUTHI LA YEMEN LARUSHA MAKOMBORA 10 DHIDI YA UWANJA WA NDEGE WA SAUDI ARABIA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 26, 2019

KUNDI LA WAASI LA HOUTHI LA YEMEN LARUSHA MAKOMBORA 10 DHIDI YA UWANJA WA NDEGE WA SAUDI ARABIA

  Malunde       Monday, August 26, 2019
Kundi la waasi la Houthi la Yemen limesema lilirusha makombora 10 dhidi ya uwanja wa ndege wa Jizan nchini Saudi Arabia jana usiku.


Taarifa iliyotolewa na mtandao wa kituo cha televisheni cha al-Masirah kinachomilikiwa na kundi hilo imemnukuu msemaji wa jeshi la waasi hao Yahya Sarea akisema, makombora 10 aina ya Badr-1 yamerushwa kwa pamoja dhidi ya uwanja wa ndege wa Jizan, na yamelenga ndege za kijeshi na helikopta za kivita aina ya Apache ndani ya uwanja huo, na kwamba askari kadhaa wa Saudia wameuawa kwenye shambulizi hilo.

Pia amesema, jeshi la Houthi litafanya mashambulizi mengi zaidi katika kipindi kijacho.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post