JELA MIAKA 30 JELA KWA KUBAKA MWANAFUNZI MWENYE UMRI WA MIAKA 17 NA KUMPA MIMBA

NA SALVATORY NTANDU

Mkazi wa kijiji cha Mpunze Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ramadhani Mohamedi (23) amekuhumiwa kwenda jela miaka 30 na Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa kosa la  kubaka na kumpa mimba mwanafunzi (17).

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo na kusema kuwa Mahakama imeridhika na Ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri ambao umemtia hatiani Ramadhani pasipo shaka yeyote.

Amesema Mahakama imepitia ushahidi wote wa upande wa jamhuri na kujiridhisha kuwa anahatia ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo hivyo atatumikia adhabu hiyo ili iwefundisho kwake na kwa watu wengine.

Awali akisoma shauri hilo Mahakamani hapo Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Evodia Baimo amedai kuwa Ramadhani katika kosa la kwanza la ubakaji amekiuka kifungu namba 130 (1) (2) na 131 (1) sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Kosa la pili Ramadhani amekiuka kifungu 60 (a) (3) sura ya 353 ya sheria ya elimu ya mwaka 2016 na kuimba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwake ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Ramadhani alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza hoja ambayo imetupiliwa mbali na Mahakama.

Tayari ameshaaanza kutumikia adhabu yake na haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ipo wazi ndani ya siku 60.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527