IKUPA: ANAYEPINGANA NA MAGUFULI ANAPINGANA NA MUNGU MWENYEWE

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Naibu Waziri kutoka   Ofisi ya Waziri mkuu,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa  amewataka watanzania kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwa ni Pamoja na Kupiga vita Dawa za kulevya na kuwezesha wenye Ulemavu.

Mhe.Ikupa amesema hayo  jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.

Ikupa ametaja Nyanja mbalimbali ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi,Uimarishaji wa Miundombinu ikiwa ni pamoja na Umeme,Barabara,Reli,Afya,Elimu bure  na Usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi  wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.

Kwa upande wao Mjumbe wa Kamati kuu  Hadija Shalo [Keisha] na mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza  Rais Magufuli pamoja Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku wakiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527