KAULI YA MTOTO WA DEREVA ALIYEGONGESHA GARI LA MKUU WA MKOA KABLA YA KUFARIKI

Na Beldina Nyakeke - Mwananchi
Muda mfupi kabla ya kifo cha Kasobi Shida (26) aliyefariki usiku wa kuamkia juzi Jumatatu Agosti 5, 2019 katika hospitali ya Mkoa wa Mara alitaka baba yake asishtakiwe kwa kosa lolote badala yake yeye ndiye achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Kasobi, mtoto wa Shida Masaba (55) ambaye ni dereva wa mkuu wa mkoa wa Mara alipata ajali Agosti 4, wakati akiendesha gari linalotumiwa na baba yake kumuendesha mkuu huyo wa mkoa.

Akizungumza na Mwananchi jana katika hospitali hiyo mmoja wa maderava wenzake na baba wa marehemu ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema kuwa alifika hospitalini hapo juzi kumjulia hali dereva mwenzie (Masaba) pamoja na kijana wake kufuatia ajali hiyo.

Dereva huyo alisema pamoja na maumivu aliyokuwa nayo kijana huyo akiongea kwa taabu alisema baba yake hastahili kuadhibiwa kwavile hakujua kama angechukua gari na kuliendesha.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527